Mpendwa mgeni uliyetembelea tovuti hii, karibu sana kwenye tovuti ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Bagamoyo. Kanisa la Waadventista wa Sabato Bagamoyo lipo katika mji wa Bagamoyo, wilaya ya kiserikali ya Bagamoyo ndani ya mkoa wa Pwani. Kanisa la Bagamoyo lina makundi ya Sayuni na Makurunge chini ya usimamizi wa Mchungaji Temba ambaye ndiye mchungaji wa mtaa wa Bagamoyo kwa sasa . Kwenye tovuti hii utajipatia maarifa yatakayokuimarisha kiroho, kiakili, kimwili, na kijamii. Tovuti hii itakukutanisha na Rafiki yako Kipenzi Yesu Kristo aliyetoa maisha yake kwa ajili yako. Yeye anakupenda na sasa yupo mbinguni akikuandalia makao na akisha kukuandalia, atakuja tena ili akukaribishe kwake. Tovuti hii imeundwa na kumilikiwa na Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni chini ya Fildi ya Pwani ya Mashariki mwa Tanzania na chini ya Union Misheni ya Kusini mwa Tanzania. Tovuti hii itakuhabarisha, itakuburudisha na kukuelimisha kwa nia ya kuboresha maisha yako na kukupa fursa ya kujiandaa Kurudi Nyumbani Kwetu Mbinguni. Karibu sana na Mungu akubariki!